SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Februari 2017

T media news

BAADA YA KUSAINI UMG: MASHABIKI WA DIAMOND WALALAMIKIA MFUMO MPYA WA KUTOA NGOMA


Baada ya Diamond kusaini mkataba na record label ya Universal Music Group (UMG), baadhi ya mambo yameshaanza kubadilika, na baadhi ya mashabiki, hususan wale wa Tanzania hawana furaha.

Of course, kuna mjadala mwingi kuhusiana na ‘kusainishwa kwake’ hasa kwasababu aliwahi kudai kuwa hawezi kuwa chini ya label, labda kama itakuwa ni partnership.

Hata hivyo kwenye mahojiano yake na Clouds FM, Novemba mwaka jana, Diamond alisema Universal Music Group walitoa dola milioni 1 (takriban shilingi bilioni 2.2 za Tanzania) kumsainisha mkataba wa kusambaza nyimbo za wasanii wa label ya Diamond Platnumz, WCB. Naye meneja wake, Sallam aliiambia Bongo5 kuwa mkataba huo ulisainiwa tangu July mwaka jana, lakini tangazo rasmi limetolewa, Alhamis hii, Feb 2.

Kwakuwa sasa UMG imechukua usukani rasmi kwa kusambaza nyimbo za Diamond, mashabiki wake wanapaswa kutambua kuwa, baadhi ya mambo yatabadilika. Kwa sasa nyimbo zake zitakuwa na mlolongo mrefu kutoka na sio kama zamani ‘click link kwenye bio kuona video yangu Youtube.’ Mfano sasa, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, ilianza kwa kuchezwa Trace TV, ambayo tunajua kuwa inapatikana DSTV pekee, hiyo ina maana kuwa hadi sasa ni Watanzania wachache wamekwishaiona.

Kwasababu lengo la UMG ni kumpeleka Diamond mbali zaidi kimataifa, Marry You unakuwa wimbo wake wa kwanza kuwekwa kwenye platform za kustream muziki kwa kulipia, ambako shabiki wa kawaida wa Masasi au Njombe, nyingi hawajawahi kuzisikia, lakini yule wa Stockholm, Sweden ndio maeneo yao ya kujidai, tayari anaufurahia wimbo huo.

Bila shaka, lengo la UMG sasa ni kumpatia Diamond mashabiki wapya wa kimataifa kumuongezea wigo wa kupata fedha za kigeni na hivyo kukuza mapato yake ambayo yataisaidia pia UMG kurudisha gharama zake za uwekezaji kwa kumsainisha, sababu hii ni biashara, sio charity. Kwa mtazamo huo, kipaumbele cha UMG kwa kazi za Diamond, sasa kitakuwa si Tanzania tu, bali kimataifa zaidi, huo ni ukweli ambao mashabiki wanapaswa kuutambua.


“Jmn simbaaaa mbona sio kma tulivyozoeaaaaa me naingia hzo option ninazoziona zte najaribu kufanya lkn cfanikiwi kuangalia why jmn,” amehoji shabiki wake mmoja.

“Yaani kwakweli umenikomesha,” ameandika mwingine. “Hayo ma vevo hata sijui niyapate wapi maana nimeenda huko stream sjui naletewa audio… Nzuri hadi vinyweleo vinanisimama… S nikaanza kutafuta video huko huko sioni popoteeeee…. 😖😖😖😖😖,” ameongeza.

Shabiki mwingine ameandika: Kuwa makini nabmashabikibzako hatabkama upo kibiashara sio kututesa kiivyo vikwazo kibao vya kuupata huo wimbo maana yake nini sasaa? VEVO ukiingia haupatikaniki ukija huku empty, YouTube empty, google empty, kuna wengine hatuna king’amuzi chenye Trace Africa hata kama tuna shida ya kuutizama wimbo wako sio kututesa kihivyo, thamini mashabiki wacha nlalamike maana bandle langu nimenunua juz GB1 niliposkia unaachia wimbo wako nmekesha online mpa kasasa nina MB9tu! Mbona unatutesa mashabiki zako na jinsi tunavyoona vipande vipande insta wewe unafkir tutakuwa na hamu nayo kama mara ya kwanza tena? Sio kihivyo brother.”

Well, hakuna ubishi kuwa wengi wana hamu ya kuiona video hii, hasa kwakuwa wimbo huu una takriban miaka 2 tangu ufanyike, lakini mashabiki wake wanapaswa kukubaliana na ukweli kuwa kama UMG ndio imeshika usukani wa kusambaza nyimbo zake, basi wajiendae kuona mabadiliko kiasi na kumkosa yule Diamond wa vitu vya fasta fasta, kitu kipo Youtube!

Huko nyuma, Diamond alikuwa na msimamo wa kutosainishwa na label yoyote labda kama mkataba ukiwa ni wa usambazaji pekee wa nyimbo za wasanii wa label yake, ambao UMG ndio inasemekana umempa. Roc Nation ni miongoni mwa label kubwa duniani zilizowahi kumtaka imsainishe lakini akazichomolea.

“Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond hivi karibuni kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.

“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”

“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine Diamond alidai kuwa kwenye album yake ijayo kuna nyimbo atakazowashirikisha Rick Ross na Rihanna.