Arsenal "walisambaratika kiakili" wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora mikononi mwa Bayern Munich, meneja Arsene Wenger amesema.
Gunners walilazwa 5-1 uwanjani Allianz Arena.
Mabao mawili walifungwa kipindi cha pili baada ya kumpoteza beki wa Laurent Koscielny aliyeumiwa.
Hii inawaweka hatarini ya kuondolewa tena hatua ya muondoano kwa msimu wa saba mtawalia.
"Ni vigumu kueleza," Wenger aliambia BT Sport.
"Muda mfupi kabla ya mapumziko, tulikuwa na nafasi mbili nzuri za kufunga. Tulirejea na kucheza vyema.
"Kipindi cha pili, tulimpoteza Koscielny upesi - alitoka tukiwa 1-1 - na hatimaye tukasambaratika. Bayern ni timu nzuri kutushinda vpia.
"Nilihisi bao la tatu liliangamiza wachezaji wetu kabisa kwa sababu baada ya hapo hatukuweza kujibu tena.
OLIVERKAYTIMES
Arjen Robben aliwaweka Bayern mbele, lakini Arsenal wakasawazisha kupitia Alexis Sanchez aliyefuatilia penalti yake ambayo ilikuwa imekombolewa na kipa.
Kipindi cha pili, Gunners waliporomoka, Bayern walitamba kwa dakika 10 ambapo Robert Lewandowski alirejesha uongozi wa Bayern kabla ya Thiago Alcantara kufunga mabao mengine mawili.
Nguvu mpya Thomas Muller alifunga bao dakika za mwishomwisho.
Alipoulizwa iwapo Arsenal wanahitaji "muujiza", Wenger alijibu: "Bila shaka".
Mfaransa huyo alijibu maswali matatu pekee katika kikao chake na wanahabari baada ya mechi, ambacho kilidumu chini ya dakika tatu.
Kuhangaishwa kwa Arsenal
3+ - Mabao ambayo Arsenal wamefungwa mechi zao nne kati ya sita za mkondo wa kwanza walizocheza karibuni hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Huu ni msimu wa kwanza kwa Carlo Ancelotti kama meneja Bayern Munich
4 - Ni mara ya kwanza kwa Arsenal kufungwa mabao manne katika kipindi kimoja tangu mechi yao dhidi ya Chelsea Machi 2014.
5 - Ni mabao mengi zaidi ambayo Arsenal wamefungwa mechi ya mkondo wa kwanza ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
8 - Bayern wamefunga mabao manane mechi zao nne zilizopita dhidi ya Arsenal Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
25.8 - Asilimia ya udhibiti wa mpira wa Arsenal wakati wa mechi yao dhidi ya Allianz Arena Jumatano.