SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 27 Januari 2017

T media news

HII NDIO SABABU ILIYOMFANYA RAPA AY KUJIFANANISHA NA MASTAA HAWA

Rapa AY amefunguka na kusema kuwa siku zote moyo wake upo kwa ajili ya ku'share vitu na watu na kuona watu mbalimbali  hata nje ya muziki wanafanikiwa kwani anaamini kufanikiwa kwake ni kuona watu wengine pia wanafanikiwa na kupiga hatua za maendeleo

AY amesema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema siku zote amekuwa akimtazama sana Dr. Dre namna anavyoweza kuwasaidia watu na namna anavyofanya kazi zake, pia anasema alijifunza kwa D'Banj namna ya kuwasaidia wasanii wengine wa nyumbani.

"Mimi nipo inspired sana na Dr. Dre, ukimuangalia Dr. Dre ni mtu ambaye ametengenezea watu wengi sana connection, kwa hiyo mara nyingi huwa naangalia jinsi anavyofanya mambo yake, ingawa mimi si producer lakini kuwafungulia njia watu wengine ni kitu nachofanya. Mimi nimeumbwa hivyo napenda ku'share na watu kitu ambacho naona hata hakitanifaa mimi basi kikufae wewe na mwisho wa siku mimi nitasema hii ni Legacy yangu nimekupatia" alisema AY 

Mbali na hilo AY anasema siku zote anapotoka kwenda nchi za watu huwa anahakikisha anabeba CD za wasanii mbalimbali kutoka Tanzania 

"Nikiwa na safari nakwenda sehemu yoyote ile nje ya Tanzania huwa nabeba nyimbo zozote zile bila kujali huyu ni nani huyu ni nani nazisambaza na hiyo kitu nilijifunza toka kwa D'Banj. Alivyokuja hapa kwa mara ya kwanza alikuwa amekuja na ma-CD kibao ya wasanii, nikajaribu kuangalia labda anakuja na Cds za wasanii wa label yake tu nikaja kugundua hapana anatembea na Cds za wasanii mbalimbali ambazo ni hits song za kule anakuja anasambaza huku kwa hiyo hata mimi nikiwa nakwenda sijui Kenya, sijui Uganda na nchi nyingine naendaga namwaga sumu tu kule, lengo na madhumini tuwe wengi" alisema AY