Usiku wa January 21, 2017 mshambuliaji wa kitanzania Mbwana Samatta aliisaidia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa ugenini dhidi ya AS Eupen kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji (Jupiler League) na kufanikiwa kuchomoka na pointi tatu za ugenini.
Ikiwa ni dakika za lala salama (82′) Samattaaliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ruslan Malinovskiy na kuiandikia bao Genk ambalo lilidumu kwa dakika zote zilizosalia.
Ushindi huo umeifanya Genk ifikishe pointi 31 baada ya michezo 21 sawa na Standard Liege ambayo imecheza mechi 20 hadi sasa, Genk inakaa nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya Ubelgiji kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Standard Liege.