SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 21 Januari 2017

T media news

Diamond Asaini Bonge La Dili, Ni la Mamilioni Ya Pesa.

Diamond Platnumz ametoka kusaini endorsement deal nyingine inayovujisha udenda mdomoni (mouth-watering deal).

Mambo yote yamefanyika Ijumaa hii kwenye ofisi zake. Wakati Donald Trump akisherehekeaa kuapishwa Rais mpya wa Marekani, Chibu alikuwa makao makuu ya WCB na uongozi wake wakisherehekea kusaini deal hilo.

“Jus Pined out! Another deal today! Thank you God for the #Blessing,” aliandika kwenye video aliyoiweka Instagram.

Bado haijajulikana ni deal na kampuni gani, lakini kwa sherehe hizo, hakuna shaka linaongezeka kwenye orodha ya mikataba yake minono aliyonayo ikiwemo ya Vodacom, DSTV na Coca-Cola.