SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 26 Novemba 2016

T media news

UPUNGUFU wa Marubani Waikwamisha Air Tanzania

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limekiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshwaji wa ndege wakati wa kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

Akizungumzia changamoto hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Mhandisi Emmanuel Korosso, amekiri kuwepo kwa changamoto ya marubani ikizingatiwa mpaka sasa shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

Amesema kuhusu wafanyakazi, bodi yake imeagiza menejimenti ya shirika hilo kusimamia kusimamisha kwa muda mktaba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso (Katikati) akizungumza na wanahabari leo.

Aidha, Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo kutangaza mara moja nafasi zote za wakurugenzi na pia nafasi za mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na bodi huku ikiwaondoa katika nafasi zao wakurugenzi wote ispokuwa Mkurugenzi Mtendaji kutokana na utendaji dhaifu pamoja na kutokuwa na sifa stahiki za elimu za kushika nafasi walizonazo.