Asha Baraka akitangaza siku ya kuzaliwa ya mmoja wa mashabiki wa bendi hiyo ambaye alikuja na keki iliyoliwa ukumbini hapo.
Dada Asha Baraka (kushoto) na Mama Wema wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati mambo yakiendelea.BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, usiku wa kuamkia jana Jumapili ilifanya onesho ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar, sambamba na mkali wa muziki wa singeli maaruu kwa jina la Sholo Mwamba.
Katika onesho hilo mambo kadhaa ya kiburudani yalijili. Angalia picha.
Khalid Chokoraa na Otilia Boniface wakicheza kimanjonjo sambamba na wanenguaji wengine.
Miraj Shakashia ‘Shakazulu’ akichagiza kwa gitaa.
Wanenguaji wa kiume kazini.
Mashabiki hawa wakifanya nao mmh!
Rapa Saulo John ‘Ferguson’ (kushoto) na muimbaji Kalala Junior wakinogesha mambo.
Pedeshee, Rehema Kiluvia akiwatunza wanenguaji.
Mkaza vitanda maarufu Dar, akiserebuka sambamba na manenguaji wa Twanga.
Sehemu ya mashabiki wakifutilia burudani.
Wanenguaji wa Twanga waliokuwa wakipiga mzigo Uarabuni kwa muda, Hamida (kushoto) na Fasha Joshua wakionesha mavitu ya Uarabubuni baada ya kurejea.
Mama Wema, Bi Mariam Sepetu nae alikuwepo kwenye onesho hilo, hapa akiwapa zawadi wadada walipendeza na vazi la kijora.