SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

T media news

Simba SC yakubali kutekeleza agizo la BMT

Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kupokea agizo lililotolewa na Baraza la Michezo La Taifa kwa mikono miwili linalohusu kufuatwa kwa mlolongo wa katiba, ili kukamilisha taratibu za mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katibu mkuu wa klabu ya Simba Patrick Kahemele amesema mpaka sasa wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha mchakato wa mabadiliko na wanaamini agizo la BMT watalifanyia kazi.

Katika hatua nyingine Patrick Kahemele amesema ameainisha hatua ambazo zitaanza kufanyiwa kazi siku za karibuni, baada ya kumaliza taratibu za awali kwa ajili ya kukamilisha dhana ya mabadiliko ya mfumo wa hisa