Msanii wa bongo fleva, Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na kolabo ya wimbo wa ‘Kajiandae’ aliyofanya na Ali kiba tena, ametoa sababu ya kuamua kufanya tena kollabo na msanii huyo.
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Ommy Dimpoz amesema mara ya kwanza alivyofanya kollabo ya Nai Nai na Alikiba ilikuwa ili atoke kimuziki, lakini kollabo ya sasa ni kama tu collabo zingine, na sio kumtumia kurudi kwenye game.
“Nai nai ilikuwa mimi nimemshirikisha Ali, nilikuwa natafuta njia ya kuuona ugali, lakini sasa hivi tumekuja kama Ali na Ommy kazi ya pamoja, mimi nilikuwa zangu break, nimerudi kwa hiyo haijalishi nimeimba na nani”, alisema Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz alishawahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wa ‘Nai nai’ ambao ndio ulimtambulisha kwenye ulimwengu wa bongo fleva, na sasa kaamua kurudi na kazi nyingine akiwa na alikiba pia, inayoitwa ‘Kajiandae’.