Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete (kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Mwakilishi wa Millen Magese group company Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma(katikati) akitoa maelezo kuhusu mashindano ya Urembo ya Afrika kwa mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga ( katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kumpata mshiriki wa mashindano hayo kutoka kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Julietha Kabete (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 yatakayofanyika nchini Nigeria kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga .
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete Mrembo anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss afrika 2016 nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete Mrembo anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss afrika 2016 nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Julietha Kabete Mrembo anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss afrika 2016 nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Na Shamimu Nyaki WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.
Mhe. Nape ametoa ahadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Mhe Nnauye ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija kwa Taifa hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini” alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“ kwa niaba ya Millen Magese group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika mashindano haya”Alisema Bw. Chuma.
Kwa upande wake Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi kuitangaza nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika urembo” Alisema Bi Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.