SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 10 Novemba 2016

T media news

MWANAMUZIKI MAARUFU SANA WA ZAMANI NCHINI AIBUKA NA KUWEKA WAZI KUHUSU TUHUMA ZA KUWA NA UKIMWI SOMA HAPA LIVE!!


Msanii mkongwe wa muziki nchini Tanzania Mr. Nice ameibuka na kusema
kuwa hana maradhi ya UKIMWI kama wengi walivyokuwa wanamzushia ila kilichomsumbua mpaka kufikia kulazwa mahututi hospitali ni kulishwa sumu wakati wa Kampeni katika uchaguzi wa mwaka jana.

Mr Nice ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na Gazeti la Taifa Leo la nchini Kenya lilifanya naye mahojiano wiki hii katika moja swali ambalo aliulizwa ni kuhusu tetesi ambazo zimesambaa nchini humo kuwa ana HIV.

Mr Nice ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, alikanusha uvumi huo huku akieleza nini kilimkuta mwaka jana mpaka akalazwa hospitali kwa miezi kadhaa.

“Kaka wewe mwenyewe ukinicheki nilivyo fresh nina ngoma kweli?,” Mr Nice alimuuliza mwandishi huyo huku akichek. 

“Siugui Ukimwi lakini ni kweli mwaka jana nililazwa hospitali kwa miezi mitatu kuanza October. Nililishwa sumu kali wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hatukuweza kubaini ni nani alifanya hivyo lakini tulijua ni mambo ya siasa na nikamwachia Mungu.

Kwa sasa Nice afya yake imerejea kama kawaida na anaendelea na kazi zake za muziki nchini Kenya.

Katika hatua nyingine amesema Tanzania kuwa na wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 kuliko jirani zake Kenya na Uganda kulitokana juhudi za msanii moja moja.

“Kusema kweli wasanii wa Tanzania wamekuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri kuliko mwenzake. Kwahiyo binafsi naona hii hali imesaidia kuwajenga wasanii wa Tanzania pamoja na muziki kiujumla,”.

Source: Bongo 5