SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

T media news

Mbowe Adai Wabunge wa CCM Wamehongwa Sh Million 10 Kila Mmoja Kupitishwa Mswada wa Habari

BUNGENI: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amedai Wabunge wa CCM wamehongwa Shilingi Milioni 10 kila mmoja ili wasaidie kupitisha Muswada wa Habari.

Mbowe amesema kikao hicho kilifanyika mnamo tarehe 25/10/2016 saa mbili usiku na kiliongozwa na Waziri Mkuu akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana.

Mbowe aliyasema hayo akimuuliza swali la papo kwa hapo Waziri Mkuu, hata hivyo swali hilo lilikataliwa na Naibu Spika kwa madai kuwa sio la Kisera.