SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 1 Novemba 2016

T media news

MATAPELI WATUMIA JINA LA MKUU WA MKOA MH MAKONDA KUTAPELI MAMILIONI YA PESA


Jeshi la Polisi kanda Maalum dsm linawasaka kundi la matapeli ambalo limetumia jina la Mkuu wa mkoa wa DSM Paul Makonda kutapeli kampuni ya kichina ya Jensen Huang kiasi cha Dola 8500 pamoja na Shilingi million 15 ambazo matapeli hao walijitambulisha kuwa wanataka kuwasaidia watoto kwa ajili ya kuwapeleka nje ya nchi kwa masomo, huku wengine wakitapeliwa dola 5000 kwa kutaka kupatiwa vibali ya kuishi nchini.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum Simon Siro Akizungumza na waandishi wa habari amesema Mtandao huo hatari wa Utapeli umekuwa ukitumia majina ya Viongozi mbali mbali kutapeli huku wakitumia baadhi ya wafanyakazi wa mabenki kufungua akaunti feki kufanikisha utapeli huo.

Katika kupambana na Uhalifu Jeshi la Polisi linawashikiria watuhumiwa wa uhalifu 220 wakiwemo majambazi wa kutumia silaha,vijana wa panya road ,watuhumiwa wa shehena za bangi zilizowekwa katika mabegi mithiri ya Nguo na magunia huku akiwapongeza wananchi wa mbagala kwa kuwashambulia wahalifu na kukamata bunduki aina ya smg na risasi 17.

Matuhumiwa wengine wanaoshikiliwa ni pamoja na wezi wa magari, vpuri mbali mbali vilivyoibwa lakini pia madumu ya mafuta ya kula zaidi ya 1000 yaliyokamatwa katika bandari bubu ya mbeweni yakitokea Zanzibar bila kulipiwa Ushuru.