Na Erick Evarist | Risasi Jumamosi:
WASANII wa Marekani walitangulia kwa muda mrefu kabla wasanii wetu wa Bongo Fleva hawajaanza kuimba. Pamoja na majumba ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali, miongoni mwa mambo ambayo waliyafanya baada ya kufanikiwa kimuziki ni pamoja na kumiliki magari ya kifahari.
Kibongobongo pia, wasanii wetu nao hawapo nyuma. Baada ya kuanza kupata mafanikio, wapo wasanii walioonesha heshima kwa kununua magari ambayo kwa levo yao tunaweza kuyaita ya kifahari.
Jide
Ifuatayo ni orodha ya magari wanayoyamiliki baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva yakiwa na makisio ya gharama za kila gari husika:
MADEE: Toyota Harrier Lexus (Sh. Mil 25-30)
DIMPOZ: Toyota Prado Short Chassis (Sh. Mil 30-35)
DIAMOND: BMW X6 (Sh. Mil. 100-140)
SHETTA: Toyota Harrier Lexus (Sh. Mil. 25-30)
MWANAFA: Toyota Mark X (Sh. Mil 18-20)
AY: Range Rover (Sh. Mil. 100- 140)
JIDE: Range Rover Evog (Sh. Mil.100-130)
JUX: Nissan FUGA (Sh. Mil.20-25)
NAY WA MITEGO: Toyota Prado (Sh. Mil. 35-40)
QUICK ROCKA: MERCEDES BENZ (Sh. Mil. 18-20)