SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 23 Novemba 2016

T media news

MADAKTARI BINGWA WA MOYO WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUPASUA KIFUA (CATHETERIZATION) KWA MGONJWA.

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao  kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakitoa huduma ya  matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa. Kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau, akifuatiwa na Dkt. Daniel Maclennan na kulia ni Dkt. Peter Kisenge.

Afisa Muuguzi wa  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau akiendelea na maandalizi ya kazi ya kutoa huduma ya  matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa huku Dkt. Daniel Maclennan (kulia) na  Dkt. Peter Kisenge (katikati) wakimtazama. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia hivi sasa iko katika kambi maalum ya  siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo na katika kambi hiyo wagonjwa 20 wanarajiwa kupata matibabu.

Dkt. Bingwa wa Moyo  kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia akitoa elimu kwa vitendo jinsi ya upasuaji wa  moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa unavyofanyika. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wako katika kambi maalum ya siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo ambapo kazi hiyo inaenda  sambamba na utoaji wa elimu kwa wataalamu wa ndani wakiwemo madaktari, wauguzi, wagavi na mafundi wanaohusika na utengenezaji wa mashine za kimatibabu.


Madaktari wakiendelea na  kazi ya kutoa huduma ya  matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa. Picha na Anna Nkinda – JKCI