Msanii wa muziki Linah Sanga amedai kuwa amejaribu kuzungumza na msanii mwenzake Recho ili kumrudisha kwenye nafasi yake lakini ameshindwa.
Akiongea katika kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV wiki hii, Linah amesema tayari ameshamfuata Recho mara kadhaa ili amweleze kinachomsibu lakini amekuwa msiri.
“Sisi wasanii tulilelewa kwa kushirikiana kwa kila hali na tulipenda kwa sababu kuna wakati tunaishi pamoja,tunatungiana nyimbo,” alisema Linah “Kwahiyo kwa upande wangu mimi na niseme ukweli namfutilia sana Recho, shoga yangu vipi? Mbona kimya, fanya hivi lakini huwezi kujua kwanini yupo vile na kwanini anashindwa kubadilika,”
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Upepo’ amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuweka wazi kitu kinachomsibu.