SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 1 Novemba 2016

T media news

*Habari za leo rafiki yangu...!!?*



Mambo yako yanakwendaje?

Leo nataka nikukumbushe kitu muhimu na kifupi sana, ambacho utakifanyia kazi siku ya leo ili kiweze kuwa na mchango kwenye maisha yako.

Leo ni tarehe *01/11/2016* hii ina maana kwamba tumebaki na siku 60 pekee kumaliza mwaka huu 2016. Siku 60 tu.

Hebu pata dakika chache leo, ambapo hutakuwa na usumbufu wowote na utafakari muda uliotumia kwa mwaka huu 2016 na siku chache zilizobaki kabla mwaka huu haujaisha.

Tenga muda huu, angalau dakika kumi tu na jiulize maswali haya muhimu sana, jipe majibu na anza kufanyia kazi.

Maswali muhimu ya kujiuliza leo zikiwa zimebaki siku 60 mwaka 2016 uishe.

*Je mwaka huu umekwendaje kwangu?*

Ufikirie huu mwaka tangu unaanza mpaka hapa ulipofika sasa, fikiria malengo na mipango uliyojiwekea kwa mwaka huu 2016. Kisha jiulize mwaka huu umeendaje kwako. Angalia ni yapi ulipanga na umeweza kutekeleza, na yapi ulipanga na umeshindwa kutekeleza.

*Unawezaje kuzitumia siku hizi 60 kuleta mabadiliko kwenye maisha yako?*

Japo zimebaki siku 60 pekee kwa mwaka huu kuisha, bado unayo nafasi kubwa ya kufanya kitu. Sasa jiulize ni kipi unachoweza kufanya ndani ya siku hizi 60 na kikaleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. Jiulize ni kipi, hata kama ni kimoja na kidogo sana unachoweza kufanya na mambo yakawa tofauti na yalivyo sasa?

*Kitu gani unaweza kufanya kila siku kwa siku 60.*

Hapa sasa, chagua kitu ambacho utafanya kila siku kwa siku 60, bila ya kuacha hata siku moja, hata kama una sababu kiasi gani za kukushawishi uache. Hebu jipe mtihani siku hizi 60, upange kufanya kitu kila siku, kila siku, usikubali kuacha hata siku moja, ni kuanzia kesho tarehe 2/11 mpaka tarehe 31/12 pekee. Hebu jaribu kitu rafiki yangu, kama utaona poa utaweza kuendelea nacho baada ya siku hizi 60, kama utaona hakikufai utaweza kukiacha, ila kwa sasa jipe siku 60 pekee.

Baadhi ya vitu unavyoweza kufanya kila siku kwa siku 60.

✅Fanya mazoezi kila siku kwa siku 60, hata kama ni kukimbia au kuruka kamba.

✅Andika kila siku kwa siku 60, changa chochote na anza kuandika.

✅Kula kwa afya kwa siku 60, bila kuharibu hata siku moja, usile vyakula visivyo vya afya kama chipsi na vingine vya aina hiyo.

✅Acha kunywa soda kwa siku 60.

✅Kama unatumia kilevi chochote, acha kwa siku 60, siku 60 tu uone.

*✅Kama kuna tabia yoyote ambayo imekuwa kikwazo kwako, hebu iache kwa siku 60.*

*✅Kama umekuwa unakosa uaminifu kwenye mahusiano yako, hebu jaribu kutofanya jambo la ukosefu wa uaminifu kwa siku 60.*

✅Kama umekuwa unagombana au kukosana na watu, hebu jaribu usiwe chanzo cha ugomvi kwa siku 60.

✅Toa mchango wako bure kabisa, uwe wa fedha, muda, nguvu, ushauri na chochote kile, kwa siku 60.

✅Unaweza kujitolea kufanya kazi ya ziada kazini kwako au kwenye biashara yako kwa siku 60.

✅Amka mapema kwa siku 60, kila siku bila ya kuacha.

✅Pangilia siku yako kabla ya kuianza, na ipitie siku yako kabla ya kulala , kwa siku 60.

*✅Dhibiti matumizi yako ya fedha kwa siku 60.*

*✅Katika siku hizo 60 kila fedha unayotumia iandike.*


✅Usiingie facebook na instagram kwa siku 60.

✅Jitoe kwenye yale makundi ya wasap ambayo yamekuwa hayana faida kubwa kwako kwa siku 60.Siku 60 tu na uone je kutakuwa na tofauti chanya au hasi kwako.

✅Soma kurasa kumi pekee za kitabu kila siku kwa siku 60. Utakuwa umesoma kurasa 600, sawa na vitabu vitatu vya kawaida.

✅Rafiki, nataka hizi siku 60 kwako ziwe za jaribio ambalo utachukua majibu na kuona kama yafaa kuendelea au haifai.

*✅Pale unapotaka kukata tamaa au kuacha, jiambie ni siku 60 tu, baada ya hapo unaweza kuendelea au kuacha.*

✅Je ni vitu gani utafanya kwa siku 60?

*MUHIMU;*ningependa nikusaidie, Hivyo nakushauri ufanye kwa siku hizi 60 na kama utakwama popote Mungu akutie nguvu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.