Inter Milan wamethibitiha kuwa wameachana na aliyekuwa kocha wao mkuu, Frank De Boer, ikiwa ni pungufu ya miezi mitatu tangu awe kocha wa Ajax.
De Boer alitangazwa kuwa kocha wa Nerazzurri tarehe Aug. 9, 24 masaa machache tangu walipoamua kumtimua kocha Roberto Mancini ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza ligi kuu ya Italia yaani Serie A.
“FC Internazionale Milano announce that they have today terminated the contract with head coach Frank de Boer,” ilisomeka hivyo kwenye mtandao wa klabu hiyo ikiwa na maana kuwa Inter Milan inatangaza kuwa imevunja mkataba na kocha mkuu Frank de Boer.
“Kikosi cha kwanza kitakuwa chini ya aliyekuwa kocha wa timu ya timu ya vijana, Stefano Vecchi, atakayekuwa kwenye benchi la ufundi katika mchezo wa UEFA Europa League dhidi ya Southampton.”
“Klabu inamshukuru Frank na benchi lake kwa kufanya kazi na klabu hii, tunawatakia kila la kheri kwa nyakati zao zijazo. Taarifa zaidi juu ya maamuzi ya kiuongozi zitaendelea kuwajia kila zitakapofanyiwa kazi.”
De Boer alipoteza michezo 7 kati ya 14 akiwa klabuni hapo huku kipigo cha 1-0 dhidi ya Sampdoria siku ya Jumapili ukiiweka klabu hiyo katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 14 pekee, zikiwa na pungufu ya 8 dhidi ya wapinzani wao AC Milan waliokuwa katika nafasi ya 3.