SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 1 Novemba 2016

T media news

MC KOBA ACHUKIZWA NA MISS TANZANIA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Koba Mc amesema amechukizwa na kusikitishwa kwa kitendo cha kupigwa kwa wingi muziki wa Nigeria kwenye mashindano makubwa ya urembo nchini  (Miss Tanzania) kuliko muziki wa wasanii wa hapa nyumbani.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Koba Mc amesema yeye kama msanii na Mtanzania pia amehisi amekosewa, kwani imeonesha ni kiasi gani hatutathmini vitu vyetu, licha ya juhudi kubwa ya wasanii wanayoifanya ya kuupeleka muziki kimataifa.

"Roho yangu imeniuma sana, na nimeamini kwa namna moja au nyingine binafsi kama msanii nimekosewa, lakini pia nimeamini kama Mtanzania nimekosewa, na naamini  wapo ambao watakuwa na mawazo na hisia kama za kwangu kwa kilichotokea katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania, lile ni tukio la kitaifa, kiukweli sioni kuwa ilikuwa ina'make sense' hata kidogo kuweza kucheza miziki ya wenzetu wa nje, sio kama tunawachukia Wanigeria, lakini kitendo cha kuplay wimbo wa Nigeria wakati tukio lile ni la kitaifa, alafu hapa Tanzania tunao muziki wetu na tunao wasanii wetu", alisema Koba Mc.

Msanii huyo aliendelea kusema kitendo kama hicho hakiingii akilini kwa sababu wao kama wao wasanii watathaminika vipi hapa nyumbani, ikiwa wanashindwa kutambulika kwenye matukio ya kitaifa kama hayo na kuwapa nafasi wasanii wa nje ya Tanzania.