SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 10 Novemba 2016

T media news

CHECK NJIA ZA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI BILA ZENGWE


Asilimia kubwa ya watu kwa sasa wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook,twitter,Instagram,Whatsapp nk na kuwa fanya mda mwingi kuwa online. Kati ya watu hawa wapo wenye kazi na wengine hawana kazi na huenda wanakuwa kwenye hii mitandao kwa ajili ya kutafuta ajira.
Je unaweza kujua kuwa kuwa kwako online unaweza kutengeneza hela na kuwa tajiri? Leo tutajifunza njia za kutengeneza kipato kwa kutumia mitandao ya kijamii au kuwa online.


Hizi ni njia tano ambazo unaweza kuzitumia na kuweza kujitengenezea kipato kikubwa.

Affiliate MarketingHii njia imewasaidia wengi na kuwafanya kuwa wanaingiza kipato kikubwa kwa kutumia mtandao wa internet. Njia hii inakuingizia kipato pale unapo peleka wateja kwenye mitandao (tovuti) wanaotoa huduma hiyo na wewe kulipwa Camission pale mteja anaponunua bidhaa kwa yule amabaye anatoa huduma ya Affiliate. Hizi ni baadhi ya mitandao ambayo unaweza kujiunga nao na kufanya biashara hiyo ya Affiliate marketing na kujiingizia kipato.
- AmazonAsociates
-Clickbank

Baada ya kujiunga nao unaweza Post bidhaa/huduma zao kupitia mitandaona kuweza kuwashawishi wateja kununua huduma au bidhaa nawewe kupata Comission yako. hii ni baadhi ya mitandao unaweza weka bidhaa zako.

-Facebook
-Blogs
-Whatsapp
-Twitter
-Instagram
2-Freelancing – unaweza kuingiza $500 – $1000
Freelancing ni moja kati ya njia ambazo zinawapatia na zimewapatia watu wengi sana kipato. Freelancing ni njia ya kujiingizia kipato kwa kutumia ujuzi wako na kuwaonyesha watu ili baadae kujiingizia kipato.
Kama una ujuzi wa SEO, SMO, content writing, Image Editing, Graphics Designing, Video Editing nk. unaweza kujiunga na makampuni yanayotoa huduma hiyo na ukajiingizia kipato.
Haya ni baadhi ya mashirika yanayotoa huduma ya Freelancing. 
Fiverr.
Upwork.
Elance.Unachotakiwa ni kujiunga na moja kati ya mashirika hayo na kuanza kuuza ujuzi wako.
3: Anza kufundisha Online:

Kama una ujuzi wowote na pia una ujuzi wa kufundisha unaweza kujiingizia kipato online kwa kufundisha. Unatachotakiwa ni kuwa na ujuzi wa kufundisha kozi kama Programming, Networking etc. Baada ya hapo unaanza kufundisha wanafunzi duniani kote kwa kutumia mitandao kama Udemy or Skillshare. Na unaweza kuingiza mpaka $100 kwa siku kutokana na utakavyokuwa unatoa huduma yako.

4- Tengeneza na kuuza Facebook Pages

Njia hii ni rahisi sana unachotakiawa ni kutengeneza FB page nzuri na kuanza kupost habari pia unatakiwa kuongeza Likes nakufikisha walau 30k Likes na zaidi baada ya hapo tafuta mteja na utaiuza kwa bei ya juu.

5- Design na Uingize Mkwanja:

Njia nyingine maarufu ya kuingiza mkwanja mtandaoni ni kwa ku Design T-shirt yako online na kujiingizia kipato kwa mauzo. Unaweza ku Design T-shirt nzuri na ya kipekee kwa kutumia misemo inayobamba na kuingiza kipato kikubwa kwa mauzo ya zile T-shirt na hii unaweza kuifanya kupitia Custom T-shirts. Unachotakiwa ni kudesign halafu kampuni itahusika kuiuza na zitakaponunuliwa wewe utapata Comission nzuri kupitia zile Tshirt ulizo design.

Natumaini mwaka 2016 utakuwa wa mafanikio makubwa na tutaacha kutumia mitandao kwa malumbano na kuigeuza njia ya kuvutia mkwanja.,

Usipitwe na hii ===> Njia ya kuongeza watembeleaji kwenye blog yako kwa kutumia Reddit