SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 24 Novemba 2016

T media news

BARAKA DA PRINCE ASEMA CHUKI NDIO INAMALIZA BONGO FLEVA

Msanii wa muziki Baraka the Prince ambaye kwa sasa yupo chini ya lebel ya Rock Star 400, ameonesha kutofurahishwa na chuki za wasanii zinazoendelea kwenye game ya muziki wa bongo fleva.

Kwenye ukurasa wake wa Instagrama Baraka ameandika ujumbe huku akiomba Mungu chuki hizo ambazo sasa zinazidi kuonekana wazi wazi ziishe.

Amesema chuki hizo ambazo zimeonekana kukuzwa sana na team za mashabiki, huku akilalamika kuwa zinachangia kuua game ya muziki wa bongo fleva.

"Mungu saidia game ya Tanzania tupendane na tuheshimiane(....)inasikitisha sana team team zinarudisha sana music industry yetu nyuma..tumekosa tunzo nyingi kubwa na za maana, sababu ya kukosa umoja na mshikamano wa mashabiki..tunatengeneza matabaka baina ya mashabiki na mashabiki...Heee Mwenyezi MUNGU ingilia kati swala hili", aliandika Baraka kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hivi sasa wasanii wengi wamekuwa wakisema hakuna chuki miongoni mwao pale zinapokuwepo tetesi, na kusema kuwa mashabiki ndiyo wanaokuza chuki hizo kupitia team zao, jambo ambalo kila siku limekuwa ni tatizo kwenye game