SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 25 Novemba 2016

T media news

Arsene Wenger amesema hakuna haja ya kupanic baada ya mechi ya PSG.


Manager wa Arsenal amewambia mashabiki wa club yake kwamba haina haja ya kupanic baada ya kutoa draw na wakiwa kwenye harakati za kumaliza juu ya group lao la UEFA.

Manager Wenger alisema,“Haina haja ya kupanic kwasababu hatujapoteza mechi lakini tumepoteza kasi ya ushindi kidogo kwenye group letu. Nadhani tuna hali nzuri kwenye timu yetu. Kwa sasa hivi tuna asilimia 90 za kumaliza nafasi ya pili na hatujapoteza mechi yoyote. Itakua mbaya kutomaliza namba moja kwenye group letu?, sijui. Kitu kinachoniumiza ni kwamba tulitakiwa kushinda mechi lakini hatujashinda “.

Mechi inayofuata ya Arsenal kwenye UEFA ni dhidi ya FC Basel ambayo itafanyika 6/12/2016 kwenye uwanja wa St Jakob Park huko Basel. Mechi iliyopita Arsenal walishinda kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Emirates.