Kocha wa Arsenal Arsenal Wenger amesema kukaa kwake muda mrefu kwenye soka kumemfunza vitu vingi sana na kutanabaisha kwamba, ili timu iweze kuwa na mafanikio inahitaji wachezaji wenye umri kati ya miaka 23 mpaka 30.
Kwa miaka mingi Wenger amekuwa akikosolewa kwa tabia yake ya kutegemea zaidi vijana kuliko wachezaji wenye uzoefu, lakini sasa amekiri kuwa timu yenye vijana wengi zaidi ni nadra sana kushinda mataji makubwa sehemu nyingi.
“Ili kuwa mchezaji uliyekamilika, unahitaji kuwa na umri wa miaka 23 kabla ya hujaafika mbali zaidi, huo ndiyo umri ambao mchezaji anaweza kuwa katika kiwango bora,” Wenger amesema.
“Unaweza kuwa na mchezaji mmoja au wawili wenye vipaji vya kipekee, kama sasa tuna Hector Bellerin na Alex Iwobi. lakini kiuhalisia wastani wa umri katika timu unapaswa kuwa kati ya miaka 23 mpaka 30.
“Kama utaangalia katika timu za taifa, huwezi kushinda mataji ukiwa na wachezaji wenye umri mdogo, kwasababu wakati mwingine inahitaji timu yenye wachezaji wenye ukomavu wa akili ili kushinda vitu vikubwa.
“Unahitaji kuwa na timu yenye uzoefu mkubwa wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.”
Jumamosi ya wikiendi hii Arsenal watakwaana na Swansea kwenye mchezo wa Premier League uatakaofayika Emirates