SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

T media news

WASHINDI WA M BET WAKABIDHIWA VITITA VYAO

 Mkurugenzi Mku wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba akizungumza kwenye hafla ya kuzawadia washindi wa M-bet jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2016.

 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi ya  fedha ya 34,179,309/= kwa  mshindi  wa M-bet, Joseph Mwakagali, (kulia) kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5,2016. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba

 Mshindi wa M-bet , Joseph Mwakagali (kulia) akishangilia mara baada ya kukabidhiwa hundi yake ya fedha ya 34,179,309/= kwenye makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa M-bet jijini Dar es salaam leo Oktoba 5,2016. Wanaofurahia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi na katikati ni  Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba.


 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi ya  fedha ya 34,179,309/= kwa  mshindi   mwingine wa M-bet, Exaud Mgeni (kulia) kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5,2016. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba

WASHINDI wawili, Exaudi Mgeni wa Iringa na Joel Mwakagali wa Mbeya, waliojinyakulia jumla ya kitita cha Sh milioni 82, wamekabidhi wa fedha zao jana katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Bosi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Abbas Tarimba.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano ya hundi yenye thamani ya fedha hizo, Tarimba aliipongeza m-Bet kwa kuendesha mchezo huo kwa ufanisi, lakini pia washindi hao kwa kuibuka kidedea.

Alisema bodi yake inafarijika kuona washindi hao wakiliingizia pato Taifa kupitia kodi watakayolipa kwa kushinda fedha hizo ambazo ni kama Sh milioni saba hivi, huku akiwataka kuhakikisha wanazitumia ipasavyo fedha hizo kuboresha maisha yao.

“Michezo ya –ku-bet’ tumeweza kuilea ili kutoa nafasi kwa wanamichezo kushiriki michezo hii ya kubahatisha ambayo ni neema kwa taifa na si janga kama baadhi ya watu wanavyodhani,” alisema Tarimba.

Alisema kwa kuonyesha jinsi michezo hiyo ilivyo na tija kwa taifa, mwaka 2014-15, ililiongezea taifa pato la Sh milioni 15 kupitia kodi, wakati mwaka uliofuata, iliingiza kiasi cha Sh bilioni 24.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kaba, alisema kuwa Mgeni na Mwakagali, walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 12 za ligi za Ulaya kwa Super 12.

“Tunafarijika kuwakabidhi kitita chao cha Sh milioni 82 Joel na Exaudi kama washindi wa m-Bet ambao kila mmoja atapata Sh milioni 41 kabla ya makato ya kodi,” alisema Kaba.

Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Super 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote kama Mgeni na Mwakagali, unaondoka na kikapu cha siku.

“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Super 1x2 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-bet,” alisema Kaba.