SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 9 Oktoba 2016

T media news

Trump kufichua kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa Clinton

Image captionDonald Trump

Mshauri mmoja wa mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ,amesema kuwa mfanyibiashara huyo bilionea huenda akatumia mjadala wa Jumatatu kuzua historia ya uhusiano wa kimapenzi wa Bill Clinton.

Rudy Giuliani amesema kuwa Trump na Hillary wana maswala katika maisha yao ya kibinafsi ambayo ni ya aibu.

Alikuwa akijibu hisia kali zilizojiri dhidi ya Trump baada ya madai ya kuwatusi wanawake.

Image captionBill Clinton na mkewe Hillary Clinton

Bwana Trump amepoteza uungwaji mkono wa zaidi ya viongozi 20 wa chama cha Republican ,wengi ambao wanamtaka ajiondoe katika kinyang'anyiro cha urais baada ya kuzuka kwa rekodi za muongo mmoja ambapo amekuwa akijisifu kuwatumia kimapenzi wanawake