SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

T media news

TFF yatoa adhabu kwa Simba kutokana na uharibifu wa uwanja wa taifa

Kamati ya bodi ya ligi ya uendeshaji imetoa adhabu kwa vilabu kadhaa kufutia vilabu hivyo kukutwa na makosa mbalimbali.

Kubwa zaidi na lililokuwa likisubiriwa ni kuona hatua gani zitachukuliwa kwa klabu ya Simba kufuatia mashabiki wake kung’oa viti wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga uliochewa October Mosi kwenye uwanja wa taifa.

Simba imetozwa faini ya shilingi 5,000,000 (milioni tano) pamoja na kulipa gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na mashabiki wa klabu hiyo.

Soma taarifa rasmi iliyotolewa na TFF kuhusu adhabu mbalimbali zilizotolewa kwa vilabu vilivyokutwa na hatia katia makosa ambayo vilikuwa vikituhumiwa nayo.