Pambano la Mbeya City vs Simba limeanza kushika kasi mkoani Mbeya baada ya Mbeya City kulalamikia kitendo cha Simba kutaka kufanya mazoezi jana jioni kwenye uwanja wa Sokoine.
“Sisi wakati tunaendelea nat mazoezi, watu wa Simba wakafika uwanjani na kuanzisha vurugu jambo ambalo lilipelekea sisi (Mbeya City) kushindwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Sokoine kwasababu baada ya mzozo ule kocha aliamua kuondoka na wachezaji wake,” anasema ofisa habari wa Mbeya City Dismas Ten alipoulizwa chanzo cha vurugu hizo.
“Ni jambo ambalo limewashangaza wengi kwa timun kama Simba na vongozi wake ambao wanafahamu kwamba taratibu za mpira ziko vipi lakini wanafanya vitu ambavyo si vya kistaarabu.”
Kwa sheria za kimataifa, timu ngeni zinatakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumiwa kwa mchezo husika siku moja kabla ya mchezo.
“Simba waliomba uwanja na mimi nikawaruhusu, lakini wakati nawasubiri wafike cha ajabu mashabiki wa Mbeya City sijui walitoka wapi wakasema Simba hairuhusiwi kuingia uwanjani. Lakini baadaye kwa busara, Simba waliamua kuondoka,” anasema meneja wa uwanja wa Sokoine Modest Mwaluka.
Ikumbukwe uwanja wa Sokoine unamilikiwa na CCM na sio Mbeya City, hivyo meneja wa uwanja ana mamlaka ya kuikodisha uwanja timu yeyote kuutumia uwanja huo ikiwa taratibu zitafatwa.