SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 12 Oktoba 2016

T media news

Sababu za legend wa Man United Eric Cantona kuwa shabiki wa Sporting Club de Portugal

Ni muda mrefu umepita tangu Eric Cantona alivyostaafu soka lakini bado anamapenzi ya dhati na mchezo huu.

Mfararansa huyo aliamua kustaafu mapema akiwa na umri wa miaka 30 na kukimbilia kwenye tasnia ya uigizaji.

Cantona alifurahia mafanikio kwenye movies za kifaransa pamoja na kufundisha soka la ufukweni (beach soccer) kabla ya kurudi kwenye soka akiwa kwenye utawala wa New York Cosmos sambamba na Pele.

Kwasasa anaishi Lisbon, mji kuu wa Ureno na amekuwa shabiki mkubwa wa soka la Ureno.

Akizungumza na vyombo vya habari vya Ureno, Cantona alisema:

“Tulipohamia hapa, nilimleta kijana wangu mwenye umri wa miaka 6 kuangalia Sporting-Benfica. Aliangalia timu zote lakini akawa shabiki wa Sporting kama mimi.”

“Niliangalia historia ya klabu, nadhani academy yao ina wachezaji wadogo wenye vipaji. Kwa upande wangu, klabu hii ni tajiri kupitia academy yao.”

Cristiano Ronaldo atakuwa na kitu cha kujivunia, kitu kingine ni kwamba wote walivaa jezi namba 7 walivyokuwa Manchester United na wote pia ni mashabiki wa Sporting.