Mwezi uliopita kulikuwa na bifu kubwa kati ya manfongo na mama yake Wema sepetu na chanzo cha hayo yote Manfongo alifunguka akisema kwamba Christian Bella alianzisha stori katika tour Bus wakati wanaelekea kwenye fiesta pande za muleba, Bella akawaambia wasanii kuwa Team Wema katika mitandao ya kijamii wanamtolea sana povu kwanini amekopi idea ya wema sepetu kwa kushilikiana na wasanii wa kisingeli katika show yake.
Sasa Movie likaanza Manfongo na wengine wakachangia ile stori, na ile stori ikamfikia mama yake wema sepetu kwa kusema kwamba Man Fongo anamjadili Wema sepetu katika Tour Bus, Sasa Perfect255 ikaona imvutie waya Christian Bella ili ijue kama ana bifu na Wema Sepetu au la.
Akiongea na Perfect255, Christian Bella amefunguka kwamba kwanza wasanii kama wasanii kutukanwa au kusemwa ovyo katika mitandao ya kijamii ni jambo la kawaida, kwahiyo labda hao ambao walikuwa wanaandika hayo mambo walikuwa hawaelewi, Bella anasema kamwe yeye hawezi kugombana na Wema sepetu kutokana na tabia zake yeye Bella na za Wema kamwe hawawezi kuja kugombana na wala hajawahi kukaa na Wema kuongelea haya mambo.
“Sisi wasanii kutukanwa katika mitandao, kusemwa au kutukosoa ni vitu vya kawaida, labda wao waliokuwa wanaandika vitu walikuwa hawaelewi, lakini mimi na wema hatuwezi kuja kugombana sidhani kama mimi na wema, kwa tabia nazomjua wema na mimi tabia zangu siwezi kuja kugombana na Wema na sijawahi kugombana naye na wala Wema hana vita na sijawahi kukaa na wema kuongelea hii ishu hata siku moja kwamba mimi nina tatizo.kwahiyo Mimi ukija kwenye Page yangu kuleta vitu vya kijinga mimi nakufuta Comment na nakublock kabisa…mimi kwangu sipendi uchafu.nafuta nablock, nafuta na block” Alisema Cristian Bella