Mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya lawama anazotupiwa kwa kiwango chake kibovu anachokionyesha klabuni hapo tangu asajiliwe msimu huu kwa kiasi cha paundi milioni 89 kilichoweka rekodi ya dunia.
Pogba ameiambia French TV kuwa anahitaji muda ili aweze kuzoea mazingira ya uchezaji ndani ya timu hiyo.
“I will need a little time to adapt in Manchester, time for the machine to start working. I am adapting, People like to talk about Paul Pogba. The critics, they stay for a day, then after that I put my music back on, I dance,” amesema Pogba.
Mpaka sasa Man United inashika nafasi ya saba kwenye ligi kuu ya Uingereza huku usiku wa Jumatatu hii timu hiyo itakuwa ugenini kwenye uwanja wa Anfield kucheza na Liverpool kwenye muendelezo wa ligi kuu ya nchini hiyo.