Loe Messi anataka kipengele cha kumruhusu kuihama Barcelona kwenye mkataba wake mpya.
Hata hivyo mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or hatarajii kuihama Barcelona hivi karibuni, anataka kuhakikisha atamalizia maisha yake ya soka nyumbani kwao Argentina (muda utakapowadia) bila kuzuiwa na Barcelona.
Ku-renew mkaba wa raia huyo wa Argentina ni moja ya vipaumbele vya Barcelona kwa wakati huu.
Hata hivyo, safari hii Messi kuomba kipengele kitakachomruhusu kuondoka ‘release clause’ ni kitu kipya ambacho hakuwahi kukiomba kwenye mikataba yake iliyopita
Kwa mujibu wa Diario Gol kupitia (AS) Messi ameiomba Barcelona kuahidi kumruhusu kuondoka ili kujiunga na Newell’s Old Boys kuelekea mwishoni mwa soka lake.
Hiyo inamaanisha kwamba, star huyo hana mpango wa kuikacha Barcelona siku za hivi karibuni lakini inaonesha anataka kuondoka baadae wakati anaelekea kustaafu.
Messi anaonesha kwamba, bado ana miaka kadhaa kucheza soka la ushindani lakini ni dhahiri anahitaji kusalia Camp Nou katika kipindi hicho.
Hata hivyo, Messi anapenda kustaafia soka kwenye klabu yake ya utotoni Newell’s Old Boys ya Argentina.
Kwa maana hiyo, Messi anahitaji release clause ili kuwa na uhakika wa kuachana na Barcelona siku zake zitakapofika mwisho Camp Nou.