SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

T media news

Baada ya Yanga kutangaza kukodishwa, Baraza la Michezo Tanzania limetoa maamuzi haya…


Mohamed Kiganja-Katibu Baraza la Michezo Tanzania

Siku moja baada ya klabu ya Yanga kuweka hadharani mkataba wake wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni inayojulikana kwa jina la Yanga yetu Limited, Baraza la Michezo Tanzanzani (BMT) limevitaka vilabu vya soka nchini Tanzania hususan Simba na Yanga kufuata sheria na taratibu sahihi kabla ya kufanya mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji .

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema, Baraza la Michezo linatambua kuwa vilabu vinavyotaka kufanya mabadiliko vina malengo ya kupata mafanikio na kama baraza linabariki mafanikio hayo lakini lazima taratibu za zifuatwe ikiwa ni pamoja na wanachama wao kupata fursa ya kujadili jambo linalotaka kutokea kwenye klabu yao pamoja na kupata ufafanuzi pale inapobidi sambamba na kupatiwa elimu pale inapobidi juu ya faida na hasara za mifumo husika.

Klambu za Simba na Yanga zipo katika mchakato wa kufanya mabadiliko huku Kiganjaakisisitiza ni lazima sheria na taratibu zifuatwe ili kutawapa mamlaka ya kufanya mabadiliko hayo.

Baraza la michezo pia  limeitaka klabu ya Yanga kufuata utaratibu wa kuunda Bodi ya Udhamini,Badala iliyopo sasa ya Mpito ya Muda ili kuitendea haki klabu hiyo.