Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amefunga goli lake la kwanza tangu alipotua kwenye klabu hiyo kabla ya msimu huu kuanza alipojumuishwa kwenye kikosi cha Jangwani kikiwa kwenye michuano ya Caf.
Chirwa alifunga goli lake la kwanza dakika ya 45 wakati Yanga ikiichapa Mtibwa Sugar 3-1 ikiwa ni mechi ya saba kwa Yanga. Mzambia huyo aliunganisha mpira uliochelewa kuokolewa na mabeki baada ya kupigwa kona iliyookolewa lakini mpra ukamkuta Simon Msuva ambaye alipiga goli kwa Mtibwa na kuzua piga nikupige.
Nyota huyo alikuwa kwenye presha kubwa kutoka kwa mashabiki kutokana na kiasi cha pesa kilichotumiwa kumnunua huku akishindwa kufunga goli katika mechi zote zilizopita alizopata nafasi kuichezea Yanga.
Goli hilo litamfanya Chirwa kupunguza presha na kucheza kwa kujiamini na huenda akawa na mwendelezo mzuri katika mechi zijazo kama ataendelea kupata nafasi kwenye kikosi cha mkufunzi Hans van Pluijm.
Magoli mengine ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 68 wakati Donald Ngoma akitoka benchi alifunga goli la tatu dakika ya 80.
Goli pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 64.
Dondoo
Yanga imefanikiwa kupata ushindi tangu ilipoifunga 2-0 Mwadui FC, ilipoteza 1-0 dhidi ya Stand United, ikatoka sare ya kufungana 1-1 na Simba October Mosi.Pointi tatu za leo zinaifanya Yanga ifikishe pointi 14 sawa na Mtibwa Sugar lakini yanga inapanda hadi nafasi ya nne kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.Katika mechi 7, Yanga imeshinda mechi nne na kutoka sare mechi mbili huku ikipoteza mchezo moja.Hadi sasa Yanga imefunga magoli 12 huku yenyewe ikiruhu magoli matatu katika wavu wake.
Matokeo yote ya mechi za VPL zilizochezwa Jumatano October 12
Mbeya City 0-2 SimbaMbao FC 3-1 Toto AfricansMwadui FC 2-0 African LyonMajimaji FC 0-1 Kagera SugarJKT Ruvu 0-0 PrisonsStand United 1-0 Azam FC