Kama ulikua hujui chukua hii..!! Mwanamke raia wa Kenya anaefahamika kama Thandi Ojeer ndie aliemlipa mwanamuki Chris Brown ili ku-perfom mjini Mombasa wikendi iliyopita,kupitia kampuni yake inayofahamika kama Wale Wasee Limited,iliyondaa tamasha la Mombasa Rocks Concert.
Gazeti la Daily Nation nchini humo limemnukuu mtu wa karibu na Mwanamke huyo na kudai kuwa Thandi anadaiwa kumlipa Brezy kiasi cha milioni 90 za Kenya ambapo Mwanamuziki huyo ali-perfom kwa muda wa dakika 90 pekee.Thandi,(39),Mfanyabiashara na Mdau wa burudani nchini Kenya,alitikisa kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2014 baada ya ku-post picha mtandaoni akiwa na Rais Uhuru Kenyatta,Abu Dhabi wakitazama mashindano ya kuendesha magari ya Formula 1.
Kama haitoshi Thandi,aliwahi kutoka kimapenzi na kiungo wa zamani wa Ufaransa Claude Makelele,aliewahi kuzichechezea klabu za Chelsea na Real Madrid ambapo hata hivyo walitengana,baada ya Thandi kumfikisha Makelele mahakamni kwa madai ya kumuibia.