SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 13 Septemba 2016

T media news

Serikali Yawaita Wafanyabiashara na Mabalozi kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Kagera

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016. 

Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.

Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-

Ubalozi wa China – Milioni 100

Ubalozi wa Kuwait – Euro 10,000

Ubalozi wa Kenya- wametoa mabati na malazi

Kampuni ya China Mercharnt Group – Mil 100

Mo Dewji – Milioni 100

Toyota Ltd – Milioni 10

TBL – Milioni 100

Woolworth -Milioni 20

Sahara Tanzania – Milioni 20

Azania Group – Milioni 20

Kagera Sugar -Milioni 100 na Tani 10 za sukari

Nosime Group- Milioni 75

Tanga Cement – Mifuko 1000 ya Saruji

Reginald Mengi – Milioni 110

Protas Ishengoma- Wakili na mhanga wa tetemeko Milioni 5

GBP, MOIL,&OILCOM- Watajenga shule mbili zilizoharibika

Vile vile Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ametangaza matembezi ya kukumbuka janga hilo na kuahidi wananchi wote na mashirika mbalimbali kujitokeza katika matembezi hayo yatakayo fanyika siku ya Jumamosi asubuhi katika maeneo ya Masaki.

 

Taarifa zaidi za Matembezi haya zitatolewa katika vyombo vya habari.