Kingunge Ngombale Mwiru ni jina la siku nyingi sana katika siasa za Tanzania. Ni mmoja wa wazee wachache walioingia katika siasa wakati Tanzania (Tanganyika wakati ule) inapigania uhuru kutoka kwa mkoloni.
Picha hii inayomuonyesha Kingunge akishuka katika bajaji imezua zogo leo kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya watu wakiohoji kama hali imekuwa ngumu kwake hadi kutumia usafiri huo.
Maswali haya yalikuwa kufuatia hadhi ya Mzee Kingunge ambapo wengi wanaamini kuwa alipaswa kuwa anatembelea gari zuri la kifahari.
Lakini huenda pengine ni maamuzi yake binafsi kutumia usafiri huo kama mwananchi mwingine wa kawaida