SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 7 Septemba 2016

T media news

MR BLUE NDIO MSANII BORA WA TANZANIA.

“Mr Blue ndio msanii bora wa Tanzania” ni maneno ambayo yamezungumzwa na mshindi wa tuzo ya nyimbo bora yenye vionjo vya asili katika tuzo za Kili kwa mwaka 2015 Mrisho Mpoto.
Mrisho Mpoto aliyazungumza hayo baada ya Mr Blue kufanya vizuri sana katika majukwaa tofauti tofauti ya Fiesta msimu huu, ukizingatika kwamba Mr Blue ni msanii mkongwe katika game na anazaidi ya miaka 10 katika kazi ya muziki lakini bado hajashuka na anaendelea kufanya vizuri.
“Kusema ukweli kama kuna chchote ambacho nimewahi kukisema nyuma naomba nikibadilishe, naomba leo niseme kwa mara ya kwanza kuwa Mr Blue ndie msanii anaestahili kuwa msanii bora wa nchi yetu ya Tanzania. Mwaka wa 10 sasa na bado yuko kwenye game. Na kama hamuyaamini maneno yangu naomba mumfuatilie na ninaamini mtaungana na mimi”
Na hayo ndio maneno ambayo yalitoka kwenye kinywa cha Mrisho Mpoto akitilia mkazo maneno yake hayo.