Dar es Salaam. Wanazuoni na wataalamu mbalimbali wa uchumi nchini wamekuwa na maoni tofauti kuhusu utafiti mpya wa Twaweza, huku wakipishana kauli kuhusu hali ya demokrasia inayoendelea nchini kwa sasa.
Baadhi wamekubalina na utafiti huo, lakini wengine wanauona umekosa uhalisia katika matokeo ya majibu ya waliohojiwa kuhusu hali ya demokrasia nchini.
Profesa Benson Bana wa idara ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema anakubaliana na matokeo ya utafiti huo na kushangaa wanaohoji.
“Utafiti hukanushwa kwa utafiti, kwa kuhoji mbinu zilizotumika kama maswali yaliyoulizwa yalilenga majibu, au iwapo mwananchi alipewa nafasi ya kufikiri, kutafakari kabla ya kutoa majibu,” alisema mbobezi huyo.