SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 13 Septemba 2016

T media news

KLOPP ABADILISHA RANGI ZA NYAVU ILI LIVERPOOL WAFUNGE ZAIDI.

Imezoeleka kuwa vilabu vingi hupenda kuenzi utamaduni wake na kuhakikisha haubadiliki kwa kipindi kirefu kwa sababu ya kuwa nembo na kuhakikisha wachezaji, viongozi na mashabiki wanakuwa na imani inayofanana juu ya baadhi ya mambo yanayohusu klabu.

Miaka mingi ilikuwa imezoeleka katika uwanja wa Anfield, nyavu za uwanja huo kuwa za rangi nyekundu. Lakini ikiwa ni katika mchezo wa kwanza kwa Liverpool katika uwanja wa nyumbani tangu kutanuliwa kwa uwanja huo na kuongeza idadi ya watu kufikia 54 elfu, nyavu nazo zimebadilika.

Nyavu za uwanja huo kwa sasa ni za rangi nyeupe tofauti na ilivyokuwa nyekundu zamani. Katika makala maalumu iliyosomeka kwenye tovuti rasmi ya klabu hiyo, ilielezwa kuwa hayo yalikuwa maamuzi ya Klopp ya kiufundi.

Taarifa zinasema kuwa Klopp aliamua hivyo ili kurahihisha na kuongeza umakini wa wachezaji wake pale wanapokuwa mbele ya goli. Kiufundi kocha huyo alieleza kuwa rangi za nyavu zinavyokuwa nyekundu huku pia nyuma yake kukiwa na mashabiki wa Liverpool ambao wanakuwa na jezi za rangi nyekundu inaondoa ubora wa mchezaji kupatia shabaha zake.

Hivyo kundoa hitilafu hiyo kwa wachezaji ilitakiwa kuwe na rangi tofauti na ambayo yeye alipendekeza kuwa nyeupe. Mabadiliko haya yalifanyika kuelekea mchezo dhidi ya Leicester City ambapo Liverpool waliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Klopp anaamini kwa rangi hiyo muonekano wa magoli unakuwa mzuri zaidi.

Ikumbukwe pia, Brendan Rodgers, aliomba mwaka 2012 kuwa nyavu za uwanja huo zirejeshwe na kuwa nyekundu, yeye akitaka iwe ni alama ya kuwakumbusha wachezaji umuhimu wa klabu na historia yake kwa ujumla.

Roy Evans alikuwa kocha wa Mwisho kuamini kama Klopp ambapo mwaka 1995, alitaka nyavu zibadilishwe kutoka nyekundu na kuwa nyeupe ili kuondoa muingiliano wa rangi pamoja na zile za mashabiki maarufu kama Kop. Je ni kweli hii inaweza kuwa tiba?