Klabu ya Simba Sport Club imepata pointi 3 muhimu katika uwanja wa Uhuru katika mchezo uliomalizika dhidi ya Azam Fc.Simba walipata goli dakika ya 67 ya kipindi cha pili lililofungwa na Shiza Kichuya.Mchezo ulikuwa wa spidi ya ajabu kwa klabu zote mbili ambapo katika kipindi cha kwanza mchezo ulienda sare bila ya kufungana.Mpaka sasa klabu ya Simba ndio inayoshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom wakiwa na point 13.Kwengineko huko katika kiwanja cha Kambarage mjini Shinyanga klabu ya Mwadui imeweza kupokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Klabu ya Yanga ya mjini Dar es salaam.Magoli ya Yanga yalifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 5 ya mchezo na goli la pili lilifungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 91.