Leicester City wamerudi kwa kishindo baada ya wiki iliyopita kupewa kipigo cha mbwa mwizi na Liverpool kwa kuwafumua Burnley mabao 3-0.
Islam Slimani, nyota wa kimataifa wa Algeria aliyesajiliwa kwa paundi mil 29 kutoka Sporting Lisbon ndiye alikuwa nyota wa mchezo.
Sliman aliifungia Leicester mabao mawili huku moja wakijifunga Burnley wenyewe.
Sliman alifunga magoli hayo mnamo dakika za 45 na 48, huku Ben Mee wa Burnley akijifunga mwenyewe na kuwapa Leicester bao la tatu.
Dondoo muhimu
Islam Slimani amefunga magoli nane kwa kutumia kichwa kwenye mashindano ya ligi tu mwaka 2016 – saba alifunga wakati akiwa Sporting Lisbon ya Ureno na mawili kwa upande wa Leicester City kwenye Premier League.Mwaka huu wa 2016 Slimani amefunga magoli 22 kwenye michezo ya ligi 23.Leicester City hawajafungwa na Burnley kwenye michezo 10 mfululizo ya ligi (wameshinda mara 7, sare mara 3 na hawajafungwa).Burnley wameshindwa kufunga hata goli moja kwenye michezo sita kati ya nane ya Premier League waliyocheza ugenini.