SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Septemba 2016

T media news

HATIMAYE MKE WA MAGIC JOHNSON AFUNGUKA KUHUSIANA NA MAISHA YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI YA MUMEWE.

Wengi wanamkumbuka moja ya wachezaji bora kuwahi kugusa mpira wa kikapu, EarvinMagic” Johnson Jr ambaye alileta ladha tofauti katika mchezo huu na kuufanya kuwa wa kipekee hasa kwenye nafasi yake ya Point Guard. Kimo chake kilimruhusu kucheza nafasi zote uwanjani, na inasemekana ndiye mchezaji bora zaidi ambaye hakuwahi kutumia uwezo wakewote kwa maana ya ufungaji. Alipenda kutokuwa mchoyo na kutoa pasi nyingi kwa wenzie.

Lakini maisha yake ya katika NBA yalikatika ghafla mwaka 1991 watu wakiwa bado wanahitaji kuona ubora wake. Hii ilitokana na kugundua ghafla kuwa alikuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kutokana na changamoto ya elimu juu ya ugonjwa huu hata wachezaji wenzie hawakutaka kucheza nae.

Mapema wiki hii mkewe, Cookie Johnson amefunguka juu ya hali mbaya aliyokutana nayo baada ya mumewe, Magic Johnson,kumueleza kuwa alikuwa amepata maambukizi hayo mwaka 1991.

“Niliogopa nusura ya kufa,” mwanamama huyu aliiambia Good Morning America. “Nilijikuta nimeangukia magoti. Wote tulijikuta tumepiga magoti na tunalia pamoja, machozi yakitumwagika.”

“Sikuwa hata na muda wa kukasirika ama kuchukia kwa lililotokea kwa kuwa sikuwa najielewa, nahisi unanielewa, or na wala sikuweza hata kujiuliza maswali” aliendelea. “[Akilinii mwaangu] nikawaza, ‘masikini, pengine anaweza kufa siku za karibuni.'”

Taarifa hizi za kuhitua zilikuja ikiwa Magic Johnson yupo katika kiwango chake bora cha mchezo wa mpira wa kikapu akiwa na klabu ya Los Angeles Lakers huku pia ikiwa ni siku 45 baada ya ndoa yao. Wnandoa hao pia walikuwa wakitarajia kupata mtoto wao wa kwanza, E.J. (sasa ana umri wa miaka 24), hali iliyoweka mahusiano yao katika jaribu gumu.

“Magic alinambia, ‘Kama unataka kuondoka nakuruhusu, sikulaumu na naelewa kinachokutokea,'” “Hapo haponikamjibu, ‘Unanitania? Hapana. Nakupenda na siwezi kukuacha, nitaishi na wewe nikusaidie uweze kuishi. Tutapata namna ya kukufanya uweze kuishi na kuushinda ugonjwa huu.”

Magic Johnson naye aliongeza kuwa mkewe alikaribia kufa kwa woga kutokana na hali ya kutokujua kama mkewe na mtoto wao ambaye hajazaliwa walikuwa moja kwa moja wameathirika.

“Unajua kipindi hicho, mtu ulitakiwa kusbiri takribani siku kumi kuweza kusuburi majibu yako hivyo jambo hili lilikuwa linatia woga,” mwanamama huyu alisema kwenye maongezi hayo. “Hatimaye majibu yalitoka na tukaambiwa kama mama hakuwa ameathirika basi na mtoto yupo salama.”

Wakati wa mazungumzo hayo, Magic Johnson hakusita kumpa sifa mkewe huyo kwa moyo wa kipekee aliokuwa nao.

“Huyu mwanamke hapa,  naomba Mungu anifunulie nijue kwa sababu gani nilimuoa, na kwanini alituunganisha pamoja,” alizungumza mchezaji huyu wa zamani kwa hisia. Magic Johnson kwa sasa ni muelimishaji na mtetezi wa masuala ya utambuzi wa virusi vya UKIMWI duniani.