SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 17 Septemba 2016

T media news

AKAUNTI ZA BENKI ZA MKE WA ZAMANI WA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA ZASHIKILIWA ZIKIWA NA MABILIONI


First lady wa zamani wa Nigeria, Patience Jonathan anadaiwa kumiliki akaunti za benki zenye thamani ya dola milioni 31.5 zilizoshikiliwa kufuatia uchunguzi wa rushwa. Hatua hiyo imeyafanya makundi yanayopinga vitendo vya rushwa kutaka ashtakiwe. Mke huyo wa rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan ameshtaki kwenye mahakama kuu mjini Lagos kuomba kufunguliwa kwa akaunti tano za dola zilizopo kwenye benki ya Skype ya Nigeria.
Akaunti hizo zilishikiliwa na tume ya makosa ya kiuchumi na kifedha, July. Pia, wakili wake alituma barua kwa tume hiyo kudai kuwa dola milioni 15 kati ya hizo ni malipo toka kwa serikali ya gharama za matibabu aliyopatiwa London mwaka 2013.
Wanaijeria wamekosoa ombi hilo kwenye mitandao ya kijamii wakihoji kama alitaka kuponya dunia nzima au kununua maisha ya milele kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha.
Rais Goodluck Jonathan alishindwa uchaguzi wa May 2015