Neymar alifunga mkwaju wa penati ya ushindi wakati wenyeji timu ya Brazil ikiichapa Ujerumani kwa penati 5-4 na kushinda medali yao ya kwanza ya dhahabu kwenye soka la wanaume katika historia ya michuano ya Olympic.
Pambano hilo lilimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika za nyongeza, Neymar akiwa ameifungia Brazil bao kwa mkwaju wa free-kick kipindi cha kwanza lakini goli hilo likasawazishwa na Max Mayer.
Kwenye changamoto ya mikwaju ya penati, Ujerumani wakashuhudia penati ya Nils Petersen ikiokolewa na Weverton kabla ya Niymar kupachika penati yake ya mwisho na kuipa Brazil medali ya dhahabu.
Ushindi huo umekuja miaka miwili baada ya Ujerumani kuidhalilisha Brazil kwa kipigo cha magoli 7-1 kwenye fainali za kombela dunia mwaka 2014 hatua ya nusu fainali.
Mbele ya mashabiki 78,000 kwenye dimba la Maracana, Brazil walipata fursa ya kulipa kisasi na hatimaye kushinda ubingwa wa soka wa Olympic baada ya kupoteza fainali tatu za mwaka 1984, 1988 na 2012.
Neymar ambaye ni mshambuliaji wa Barcelona aliyeukosa mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia kutokana na kuwa majeruhi, alifungua nyavu za Ujerumani kwa mpira wa adhabu ndogo mita 25 toka langoni na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa mbele.
Mashuti matatu ya Ujerumani yaligonga mwamba katika kipindi cha kwanza kupitia juhudi za Julian Brandt aliyepiga shuti la umbali wa mita 25 huku shuti la Sven Bender likiwababatiza mabeki na kugonga mwaba kabla ya kupiga kicha na mpira kugonga mwamba kwa mara nyingine lakini wakapata bao la kusawazisha muda mfupi baada ya mapumziko.
Hakuna timu yeyote iliyoweza kupata goli la ushindi kabla ya kufika kwenye changamoto za mikwaju ya penati ambazo zilimalizika kwa Brazil kutwaa medali ya dhahabu.
Golikipa wa Brazil Weverton amesema: “Medali ya dhahabu ni yetu, lakini ni kwa ajili ya Mungu. Mungu anampenda Neymar kama anavyoipenda timu yetu.”
Neymar akaongeza: “Hiki ni miongoni mwa vitu muhimu ambavyo vimetokea maishani mwangu. Ni hivyo tu.”
Mechi ya kisasi
Miaka miwili iliyopita, wenyeji wa michunao ya kombe la dunia huku wakipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, Brazil walijikuta wakiangukia kipigo kikubwa kuwahi kukutana nacho kwenye fainali za kombe la dunia baada ya kujikuta wamechakazwa goli 5-0 ndani ya dakika 29 kwenye kichapo cha bao 7-1 kutoka kwa wajerumani.
Kabla ya fainali ya Olympic, kocha wa Brazil Rogerio Micale wanachohitaji ni ushindi na haoni kama timu yake inahitaji kulipa kisasi kwasababu hakuna mchezaji wake aliyecheza mchezo wakatim Brazil inapoteza 7-1 dhidi ya Ujerumani.
Alisema hakuna mchezaji wake aliyekuwepo kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia huku kikosi chake cha Olympic kikiwa na nafasi ya kuchezesha wachezaji watatu pekee waliovuka umri wa maiaka 23.
“That was the World Cup, this is the Olympic team,” said Micale. “Neymar never played in that match so there is nothing that could generate any type of feeling that we have to take revenge.
“It is a different time with different players and ages.”
“Wakati ule ilikuwa ni kombe la dunia, sasa ni Olympic,” alisema Micale. ”Neymar hakucheza kwenye mchezo ule kwahiyo hakuna kitakacholeta hisia za kulipa kisasi.”
“Ni wakati tofauti, timu tofauti na umri tofauti.”
Mashabiki wengi walijitokeza kuishangilia Brazil kwenye uwanja wa Maracana na walipata kile walichokitarajia kutoka kwa timu yao.”
Nigeria yatwaa medali ya shaba
Nigeria wameshinda medali yao ya kwanza kwenye mashindano ya Olympic mwaka 2016 baada ya kuifunga Honduras mabao 3-2 kwenye mchezo wa kuwania medali ya shaba ambapo Sadiq Umar alifunga mara mbili huku Aminu Umar akifunga bao moja.
Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi, aliyekuwa nahodha wa Nigeria amesema: “Nimefurahishwa na hiki kikosi, vijana walijituma sana.”
“Ni muhimu sana kwasababu mchezo wa soka unapendwa sana Nigeria. Tulikuwa na presha nyuma yetu lakini tumejitahidi tumefanya kile tulichoweza kwa ajili yetu, familia zetu na Nigeria.”