SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 24 Agosti 2016

T media news

MWAMBUSI AKUBALI YANGA IMEPATA SOMO

Baada ya kikosi cha Yanga kusukumwa goli 3-1 na TP Mazembe katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A uliopigwa mjini Lubumbashi DR Congo, kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema timu yao haijatoka mikono mitupu badala yake kuna mambo mengi ambayo wachezaji pamoja na benchi la ufundi wamejifunza kutoka katika michuano hiyo yapili kwa ukubwa katika ngazi ya vilabu baada ya ile ya vilabu bingwa Afrika.

“Kuna vitu ambavyo tumejifunza kwenye mashindano haya na tunataka tuendelee kuangalia nguvu yetu inaishia wapi ili kusudi tujipange kama benchi la ufundi pamoja na wachezaji nini ambacho tumekipata kwenye mashindano haya na nini tutafute,” amesema Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga.

“Wachezaji wetu wamejifunza na wameona mashindano haya yakoje, nidhamu ya namna gani, kwasababu mchezaji kama Ngoma amekosa mechi nyingi kwasababu ya kadi za njano ambayo inaathiri timu kwasababu michezo ipo michache na wachezaji wanahitajika wote wawepo lakini amekosa kutokana na kadi.”

“Tunajifunza mashindano yanahitaji yanahitaji utii wa sheria na mambo mengine kama kwenye ligi nyingine duniani.”