SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 3 Agosti 2016

T media news

KWANINI SANE AMEFANYA MAAMUZI YA KUTUA MAN CITY CHINI YA GUARDIOLA?


Kila mchezaji ana aina ya uchezaji ambayo humvutia mtazamaji. Na kila kocha ana aina ya mfumo ambao kuna baadhi ya wachezaji wanaweza kuendana nao na wengine kushindwa kabisa. Kuna namna mchezaji mpya wa Man City Leroy Sane anavyocontrol mpira, anavyogeuka, anavyopiga chenga. Uchezaji wake huwezi kuutofautisha na Messi au Arjen Robben. Wawili hawa wanatumia mguu wa kushoto. Sasa wanapokuwa wanashambulia kutoka kulia huwezi kuwatofautisha hata kidogo na kinda huyu wa Kijerumani.

Ukiangalia kwa namana umbali wa mpira pindi anapoukokota, nammna alivyo na control kama ana sumaku mguuni,  athari za pasi zake au mashuti anayopiga kama akipata nafasi, huu ndiyo aina ya ufundi ambao Pep Guardiola amekuwa akiutaka kujenga misingi imara kwenye timu zake, hususan kwenye timu alizopita za Barcelona na Bayern.

Guardiola ni mtu ambaye anapenda soka la pasi nyingi, hilo liko wazi, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba hapendi kutegemea zaidi ubora wa mchezaji mmoja mmoja kama ilivyo kwa mfano kwa Robben au Messi. Aina ya wachezaji ambao wana uwezo wa kukaa na mpira ndio chaguo lake kwa sababu hapendi mchezo wa pasi ndefu au counter attack.

Ukiangalia vizuri namna Guardiola alivyojenga timu zake, Barcelona na Bayern, liha ya kujenga mfumo wa kucheza kitimu zaidi lakini aliwafanya Messi na Robben kuwa bora zaidi kutokana na nmana alivyoijenga timu kupitia wachezaji hao.

Ukiangalia kwa aina ya wachezaji waliopo Man City kwa sasa ukiondoa aliowasajili, Pep angepata shida sana kutokana na ukweli kwamba mfumo wake na wachezaji waliopo ni vitu viwili tofauti. Ujio wa Ilkay Gindogan kwenye nafasoi ya kiungo na Nolito kwenye safu ya ushambuliaji unampa fursa ya timu walau kucheza kama anavyotaka.

Usajili huu wa City, pengine unaweza kuwa usajili hatari zaidi ukiangalia kwa jicho la tatu hasa baada ya kumuongeza bwana mdogo Sane. Hebu angalia kuna Sergio Aguero, Kevin De Bruyne, Nolito, Raheem Sterling na Sane mwenyewe. Hapa unaweza kuchmokea wapi?

Si rahisi kwa makocha hawa wakubwa kuona kipaji kama cha Sane isipokuwa Guardiola. Sidhani kama kuna kocha mwingine (kama wapo wachache) ambaye anaweza kubadili udhaifu wa Sane kuwa ndiyo uimara wake. Sasa Sane chini ya Guardiola atayapata haya yote.

Msimu uliopita kuna wakati Sana alipata wakati mgumu sana akiwa na klabu yake ya Schalke. Kila kitu kilikuwa ovyo kwake, alicheza michezo mingi bila ya kufunga au hata kutoa pasi ya goli. Kocha wake Andre Breitenreiter akamuondoa kwenye kikosi cha kwanza katika michezo takriban minne.

Alionekana kwenye mchezo ambao alichangia kipigo kwa timu yake pale walipofungwa 2-1 dhidi ya Mainz mwezi February. Wakati timu hizozikiwa sare ya bao 1-1, huku Schalke wakisaka ushindi kwa udu na uvumba, Sane alichukua mpira na kuanza kupiga chenga lakini baadaye akapokonywa na mpira huo kuzaa bao kwa timu yake kufungwa. Endapo wangeshinda mchezo huo wangeata nafasi ya moja kwa moja kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Haukuwa msimu mzuri sana kwake akiwa na Schalke. Ni kweli alikuwa akipiga vyenga vingi (alipiga chenga 98 ambazo zilifanikiwa), alifunga japo sio sana (magoli 8), lakini alitoa assists pia (sita). Pia kuna mapungufu aliyokuwa nayo hasa suala la upotezaji wa pasi, kukosa magoli ya wazi, na kukosa maamuzi sahihi ndani ya wakati sahihi na vile vile mashambulizi mengi ambayo yaliharibikia miguuni mwake. Lakini kwa ubora wake na ukijumlisha na uwepo wa kocha ambaye anajua matumizi ya wachezaji wa aina yake, basi tutarajie makubwa kutoka kwa kinda huyo.

Ada yake ya uhamisho hakika ni sahihi kabisa ukilinaginisha na umri wake na ubora wake, licha kwamba bado ana  mengi ya kujifunza. Kikubwa ambacho kinaonekana hapa ni kwamba Leroy Sane alimuhitaji kocha aina ya Guardiola na Guardiola anahitaji mtu kama Sane ili kutimiza azma yake kunako klabu yake mpya ya Manchester City.