Katalamu binadamu katika safari ya ukuaji hupitia vipindi mbalimabali. Katika vipindi hivyo binadamu kwa muda mwingine huwa na furaha,huzuni,wasiwasi na hofu pia. Pia ni hivi ndivyo vipindi ambavyo humsaidia kujifunza mambo mabalimbali ikiwa pamoja na tabia na mafanikio.
Hebu twende pamoja kujua na kujifunza Vipindi hivyo ni;
Umri wa mwaka (0-18).
Katika kipindi hiki binadamu huwa mtoto na anayependwa sana na wazazi wake, katika kipindi hiki mwanadamu anakua katika kipindi cha kufundishwa vitu kutoka kwa watu mbalimbali. Mfano mtoto mdogo katika hali kwa kila anachokifanya kwake huona ni sawa eidha ni jema au baya.
Mzazi huchukua jukumu la kemkekemea kama anafanya jambo baya na humpongeza pale anapofanya vizuri. Mfano mtoto hupongezwa kumsaidia mzazi kufanya kazi, kuwaheshimu watu wote, kufaulu katika masomo yake na mengineyo mengi. Kiujumla katika kipindi hiki binadamu huwa ni tegemezi kwa jamii inayomzunguka.
Kipindi cha umri kati miaka (19-35).
Katika kipindi hiki binadamu huanza kujitambua yeye ni nani.Vilevile katika kipindi hiki ni kipindi ambacho binadamu anaanza kupanga mipango mingi. Mfano katika kipindi hiki mtu huanza kupanga mambo mbalimbali nataka katika maisha yangu kitu cha kwanza kuwa nacho ni gari, mwingine utamsikia mimi nataka nianze kuwa na nyumba, wengine utasikia nataka kuolewa na mtu mwenye pesa, wapo wengine utawasika nataka kuoa mwanamke mzuri na mipango mingine mingi.
Katika kipindi hiki utawasikia wanasema ndio kipindi cha kula ujana wakiwa na maana ya kwamba ni kipindi cha kwenda kumbi mbalimbali za burudani, pia ni kipindi cha kupendeza, pia ni kipindi cha vijana wengi kujiingiza katika kuiga mikumbo kutoka kwa watu mbalimbali hatimaye kujiingiza kwenye wizi,kuvuta bangi,umalaya na mengineyo mengi. Utawasikia wengine wanakiita kipindi cha tumia pesa ukuzoee.
VIPINDI VYOTE NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA.
Dah yaani ni kipindi hiki kina mambo mengi sana. Katika kipindi hiki tupo baadhi ya watu huwa bado wapo katika kipindi cha utegemezi. Mfano mzuri ni wanafunzi wanasoma elimu za juu yaani vyuo wao huamini ya kwamba hawawezi wenyewe kusimama na kujitengeneze njia sahihi ya kujipatia kipato.Pia wanafunzi hawa kwa walio wengi huwa wanafikiri maisha baada ya elimu zao ni kuajiriwa.
Lakini ndugu msomaji wa makala hii lazima ufikiri zaidi kuajiriwa peke yake ili uweze kuona mafanikio makubwa ndani yako. kitu kikubwa ni kuwa mbunifu.Wito wangu kwako ni kwamba endapo utatumia vizuri kipindi hiki ukiwa na mtazamo chanya utapata mafanikio makubwa sana.
Umri kati miaka (36-45).
Ni aina nyingine ya vipindi ambayo hupitia mwanadamu. katika kipindi hiki ni kipindi cha utekelezaji wa yale uliyoyapanga katika kipindi ulichopita yaani cha miaka( 19-35). Katika kipindi hiki ni kipindi ambacho kina majukumu mengi ambayo yanamfanya mtu akose hata usingizi. Katika kipindi hiki mtu huwa na majukumu mengi sana kwa mfano kujenga, kusomesha watoto,huenda ukawa tegemeo katika familia yako.
Kwa kuwa katika kipindi hiki kina mambo mengi ya utekelezaji ni vema kile unachokipanga katika kipindi cha mipango yaani miaka (19-35) na utekelezaji uanza katika kipindi hicho. Nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba katika kipindi hiki cha miaka 36-45 watu wengi hujikuta wana mipango mingi lakini ugumu unakuja katika utekelezaji.
Umri kati ya miaka 46-na kuendelea
Hiki ni kipindi cha uzee ambacho mara nyingi huiitwa ni kipindi cha masahihisho. Katika kipindi hiki baadhi ya watu hupungua uwezo wa kufikiri hatimaye kuwa kama watoto. Pia Watu wengi hapa hupatwa na magonjwa mbalimbali kama pressure,figo kufeli, kisukari na mengineyo. Katika kipindi hiki watu hustaafu kazi zao. Katika kipindi hichi watu wengi hupatwa na pressure kutokana na walishindwa kupanga na kutekeleza mambo yao katika vipindi vya umri kati (19-35).
Mfano mtu alikuwa ni mfanyakazi wa serikali na hajawahi kujenga nyumba yake ya kuishi wala hana usafiri vyote alivyokuwa anatumia vilikuwa ni mali za ofisi. Inafika wakati wa kustafu anapata mafao yake ndo pale anaanza kupanga mipango yake na kujikuta hela aliyopewa katika kiunua mgongo imeisha kwa sababu mtu huyu anakuwa ana mipango mingi katika kipindi cha uzee matokeo haelewi aanze na kipi katika utekelezaji. Je, aanze na kununua gari? Je aanze na kufungua biashara? Je aanze na kujenga nyumba? Matokeo yako mipango inakuwa mingi kuliko utekelezaji hatimaye anapata pressure.
Wito wangu kwako kumbuka siku zote kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua. Katika safari ya mafanikio kila linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe kijana tambua ya kwamba muda wa kupanga na kutekeleza mambo yako ni sasa achana na usemi eti kijana ni taifa la kesho kwa kuwa ukiushika usemi huo utakuwa unachelewa katika safari yako mafanikio.
DIRA YA MAFANIKIO inakutakia kila jema katika safari yako ya mafanikio. Pia endelea kutembelea ukurasa huu kila siku ili ujifunze zaidi kuhusu mbinu mbalimbali za mafanikio.