Na Hamida Hassan
Mtangazaji wa Kipindi cha Muziki Mtamu kupitia Azam TV, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameeleza kuyachukia maisha yake ya nyuma na kusema kuwa, kila akiyakumbuka anajichukia.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Mai alisema kuwa kwenye usichana wake amepitia mambo mengi ya ajabu ambayo hatamani yajirudie ndiyo maana kila akiyafikiria hayo anakosa amani.
“Siwezi kuweka wazi maisha yote niliyopitia kwa sababu kwa sasa kwanza nina familia lakini sipendi hata kuyakumbuka, nahisi sikustahili kuwa na maisha yale,” alisema Mai.
Pamoja na mambo mengine aliyopitia mtangazaji huyo, pia aliwahi kuwa memba wa kundi lililojiita Alkaida la Bongo ambalo lilijumuisha mastaa kadhaa wa kike akiwemo marehemu Amina Chifupa na matendo yao yalikuwa ya kisharishari tu.