SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 15 Julai 2016

T media news

KITU AMBACHO MAXIME ATAHAMANACHO KUTOKA MTIBWA KWENDA KAGERA SUGAR


Kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime anasema anaimani atafanya vizuri kwenye klabu ya Kagera Sugar licha ya ugumu ambao anatarajia kuwepo kwenye ligi kuu msimu ujao.

Maxime ambaye kabla ya kuhamia Kagera Sugar alipata mafanikio makubwa na klabu ya Mtibwa Sugar, anasema ataendelea na falsafa yake ndani ya klabu hiyo.

Sports Extra ya Clouds FM imefanya mahojiano na Maxime siku chache baada ya kocha huyo kutangazwa kuhamia Kagera Sugar na nafasi yake kuzibwa na Salum Mayanga aliyeokea Tanzania Prisons ya Mbeya.

Sports Extra: Moja kati ya vitu ambavyo watu walikuwa wakivitazama sana Mtibwa ni mfumo wa kukuza na kuibua wachezaji wachezaji na hata kiwango kwenye ligi kilikuwa bora kutokana na misingi hiyo. Kagera haijaonekana kuwa na mfumo huo, unapohamia Kagera utaendeleza falsafa yako kama ilivyokuwa Mtibwa au utafata falsafa yao?

Maxime: Falsafa inakuwa ya mwalimu, naenda na falsafa yangu Kagera, kwahiyo ntawapa nafasi vijana kama nilivyokuwa nafanya Mtibwa. Kikubwa vijana wanaopewa nafasi wafanye kazi.

Sports Extra: Ukitazama changamoto za ligi kwa msimu uliopita na msimu huu unaokuja, unadhani katika kipindi hiki cha maandalizi ambacho bado hujakaa na wachezaji unadhani ligi ya msimu ujao itakuwaje na utajipangaje ukizingatia utakuwa kwenye changamoto mpya?

Maxime: Ligi ni ngumu na mimi naenda kwenye timu mpya lakini sidhani kama itasumbua sana kwasababu wachezaji wengi wa Tanzania tunawafahamu kikubwa ni kufanya kazi katika misingi ambayo nilikuwa Mtibwa. Kwahiyo kile ambacho nilikuwa nafanya Mtibwa nafanikiwa, ntakihamishia Kagera na kuongeza zaidi ili tuweze kufanikiwa.

Sports Extra: Unaawaambia nini watanzania, sasa tupo katika kuutengeneza mpira na wewe tayari umeshahama kutoka Mtibwa kwenda Kagera

Maxime: Tushirikiane kwasababu siwezi kutengeneza mpira mimi peke yangu. Tutengeneze mpira kwa pamoja ili tuweze kusonga mbele.