SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 14 Julai 2016

T media news

DK. MWAKA TENA,KILICHOWAPONZA MPAKA KUFUNGIWA CHAFICHUKA,SIRI NZITO



Tabibu Juma Mwaka  

Mwandishi wetu, Amani
DAR ES SALAAM: Kimenuka! Juzi, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limekifutia usajili wa kutoa huduma za kitabibu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan kilichopo Ilala Bungoni jijini hapa, kinachomilikiwa na Tabibu Juma Mwaka pamoja na vituo vingine kama hicho, kwa madai ya kukiuka taratibu za huduma na tiba mbadala, Amani limepata kilichowaponza.


Akitangaza hatua hiyo, mwenyekiti wa baraza hilo, Dokta Edmund Kayombo alisema hatua hiyo imekuja baada ya wahusika kukiuka taratibu za huduma hiyo na kwamba, licha ya kwenda kinyume na kuonywa, baadhi yao hawakusikia.Mbali na Tabibu Mwaka, Mwenyekiti Kayombo alivitaja vituo vingine ambavyo usajili wake umefutwa, kusimamishwa au kupewa onyo kuwa ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Emily Kabujanja (kimefutiwa) na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai (kimefutiwa).

Tabibu Abdallah Mandai
Kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa na Ndulu Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Castory Ndulu vyenyewe vimepewa onyo.Tabibu John Lupimo wa Lupimo Sanitarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic wamesimamishwa kwa muda wa miezi sita.Kayombo alisema waliopewa onyo na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya matangazo.



 

Dokta Rusigwa.
KILICHOWAPONZA
Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina wa gazeti hili, kilichowaponza wahusika hao ni kukaidi maelekezo mbalimbali waliyowahi kupewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwamba wasifanye mambo makuu matatu kwenye huduma yao.
“Kwanza walia-mbiwa kuwa, wasiwe…wanavaa vile vipimo vya kutundika shingoni (stethoscope) kama madaktari. Pia waliambiwa wasijiite madaktari kwani wao ni matabibu lakini wameendelea kujiita madaktari.
“Mfano, Mwaka, kwenye matangazo yake amekuwa akisema; naitwa Tabibu Juma Mwaka, lakini wengi hupenda kuniita Dokta Mwaka. Lile ni tangazo tofauti na maelekezo. Wizara imejiridhisha na kubaini kuwa wao wenyewe wamekuwa wakipenda kuitwa madokta na si watu wanawaita hivyo.
“Kingine ni ishu ya kusema wao wanatibu kisasa. Ni kosa pia, kwani wao ni matabibu wa tiba mbadala na siyo wataalam wa tiba za kisasa. Tiba za kisasa zinapatikana hospitali tu,” kilisema chanzo hicho.Kikaongeza: “Pia wizara ina habari kwamba katika vikao vyao na mitaani wanapokaa, hawa jamaa walikuwa wakisema waziwazi kwamba hawawezi kutiii maagizo ya serikali kwani wao wana umoja wao ambao ndiyo unaotoa mwongozo.”Juzi, Amani liliwasaka wahusika hao kwa njia ya simu ili kuwasikia wanasemaje lakini simu za wote, ukiacha Tabibu Fadhili Emily, hazikupokelewa.Kwa upande wake, Fadhili alipotafutwa, alituma meseji: “Nipo kikaoni nitakupigia baadaye.”Amani lilimtumia meseji kutaka kujua uhakika wa kufutiwa usajili wake na pia nini tamko lake, lakini hakujibu wala kupiga kama alivyoahidi mwenyewe.
DALILI ZA AWALI KWA TABIBU MWAKA
Kwa Tabibu Mwaka, siku chache baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri, Hamisi Kigwangalla akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kawaida, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo chake kilichosifika kwa kutoa tiba mbadala, hasa kwa wanawake wanaosumbuliwa na matatizo ya uzazi.
Waziri Kigwangalla alitoa amri ya kufungwa kwa muda kwa kituo hicho mpaka uchunguzi wa kina utakapokamilika ili kuona kama huduma zinazotolewa zinakidhi vigezo na ni salama kwa wananchi. Lakini baadaye ilidaiwa kuwa, alikamilisha mambo yote.